USIMKOPESHE RAFIKI AU NDUGU YAKO

Kwa nini leo nimefikiria haya?  Naomba nikwambie pesa ni jawabu la mambo yote namadhambi yote yameanzia kwenye pesa.   Unaweza kuwa na rafiki au ndugu mliyeshibana sana lakini pesa ikaja kuwatenganisha kwa urahisi mno na mkachukiana milele.  Pesa inatengeza marafiki na pia inaleta uadui ndani yake.  Basi ili uishi kwa amani kila kitu unatakiwa ukifanye kwa kiasi.

Kila wakati fanya msaada wa kipesa kama zawadi usifanye kama mkopo.  Kama haujampa mtu  msaada wa kipesa urafiki wenu unaenda kuisha taratibu. Kama uko kwenye eneo la kuweza kumsaidia mtu basi msaidie usimkopeshe mpe tu.  Na kama unajua hauwezi kumpa usimkopeshe itaenda kukuumiza wewe mwenyewe

(Ron Henley).

Sababu ya kutompatia mkopo rafiki au ndugu wa karibu ni kwasababu ya kuondoa usumbufu usio wa lazima wa kudaiana pasipo mashiko. Uhusiano wenu unaenda kuvunjika kama sio kuharibika kabisa.  Sababu ya watu inayowapelekea kupata matatizo ya kipesa ni kutojua jinsi ya kufanya kazi na pesa au jinsi ya kutumia fedha.  Ukiwakopesha wala hawajui wanaenda kufanyia nini kwani hawajajiandaa cha kwenda kufanyia hizo pesa.

Kabla ya kufahamu hivyo watachukua pesa kwako tena wataanza kutoa udhuru wa kushindwa kukurudishia.  Kinachofuata hapo ni kukukimbia kila wanapokuona.  Kuacha kupokea simu yako na mwisho kutofungua mlango mara unapopiga hodi majumbani kwao.

Naomba kwa ushauri kama unataka kumsaidia ndugu yako au rafiki mpatie pesa kama msaada na sio mkopo ili uishi kwa amani kwani utakapomkopesha hiyo pesa usiihesabu katika akiba yako kwani imeondoka na hauwezi fahamu itarudi lini.

Hii ni kwa faida yako ya watu wengine.

Karibu tusaidiane pale tuliposhindwa na tunapoweza tuelekezane.

Kwani maarifa ni mali kuliko pesa.

Lusako Mwakiluma

Mhamasishaji na Muinuaji kwa waliokata tamaa na kuugua

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *