MWAKA 2022 UNA MAAZIMIO YAKE UMEAZIMIA NINI?

MWAKA 2022 UNA MAAZIMIO YAKE UMEAZIMIA NINI?
  1. Fanya mazoezi madogo madogo nyumbani kwako unapoamka 11.30asubuhi mpaka 12.00 asubuhi. Hii itakusaidia kuwa makini kichwani na mwilini, mwili unajengwa kwa fikra, mwili na akili yako.  Kama asubuhi yako itakuwa nzuri na chanya kila kitu kwa siku hiyo kitakuwa hivyo.  Jaribu sasa na utaona mabadiliko makubwa kwa mwaka huu mpya na mwenye nguvu zaidi kwako.
  2. Acha kuangalia simu yako mara unapoamka asubuhi, baada ya mazoezi ebu mtafakari Mungu wako na angalia leo itakuwaje kwa manufaa yako, familia na jamii inayokuzunguka, usipoteze muda kwenye simu hakuna jipya ila kupoteza yale uliyoyapanga. Simamia unachokiamini na tenda kwa wakati kulingana na nini kikamilike kwa siku hiyo.
  3. Tafuta chakula ambacho kitakuletea afya na nguvu pia usile bora kula hii itakuletea uzito mkubwa na kuharibu afya yako. Ukitembelea nyumba ya mtu usikaribie kila kilichoandaliwa fuata ratiba yako na fuata mlo kamili unaoutumia.  Unaweza kuwashirikisha huwa unatumia nini kuepusha kula kitu ambacho sio cha kujenga mwili na faida yako.
  4. Fanyia mazoezi kila siku kile kitu unachokipenda, mfano unataka kuwa kama Oprah Winfrey basi hakikisha kila siku unafanyia mazoezi maneno yake, matendo yake hata kama unaweza kuanzia kazi hicho unachokipenda itakujenga zaidia na utakuwa imara sana, kwani mazoezi mazuri ni yale ya kuyatendea kazi.
  5. Wafanyie watu yale ambayo unapenda kufanyiwa wewe na sivinginevyo, angalia usimuumize mtu baada ya hapo muhurumie na kumsaidia Yule mwenye shida. Dunia ni Karma kile kibaya utakachotenda kwa mwenzio kitarudi kwako kwa maumivu, kuwa makini na wale wanaokuzunguka tenda wema kasha nenda zako, wala usihesabu shukurani kutoka kwa mtu mlipaji sio wewe.

Naamini hiki ni chakula cha siku na mwaka mzima najua utashiba na mwaka 2022 hautakuwa wa hasara kwako.        Simamia njia tano ziweze kukubadilisha na kukufanya mpya wakati wote.

Dr Lusako Mwakiluma

Muinuaji na Mhamasishaji