Dr. Lusako Mwakiluma aongea kwenye Moro Career Care akizungumzia mahusiano na career
Dr. Lusako Mwakiluma aongea kwenye Moro Career Care akizungumzia mahusiano na career
Dr. Lusako Mwakiluma toka Wezesha Mabadiliko Mgeni rasmi Bright Day Care Centre-Morogoro
Kama binadamu unatakiwa ujitambue ili uweze kwenda na wakati au kufanya yale ambayo yanatakiwa kufanyika na yale ambayo hayatakiwi kufanyika usiyafanye.
Kuna mambo ya msingi ya kuyafanya ili uweze kufikiria vizuri wakati wote. Na kila mtu atakayekuona atajua huyu mtu amejitambua na amejua umuhimu wake katika jamii inayomzunguka kwani utajikubali wakati wote na kuwaheshimu wengine.
Moja
Fikiri vizuri (jenga mfumo wa kufikiri vizuri); mfumo huu uwe endelevu; siyo usubiri upate tatizo ndiyo uanze kufikiri vizuri (usiwe kama zima moto). Hii itakusaidia kuanza kupanda mbegu njema kwenye mawazo yako ya kina ili maisha yako ya baadaye yawe mazuri; yatoe mbegu nzuri/njema.
Mbili
Rudisha mawazo yako nyuma, jenga picha yako ya utotoni. Chagua taswira moja wakati ulipokuwa mtoto jione kimwili, kimavazi na mazingira ulipokuwa (nyumbani /shuleni au popote). Kisha rudi kwako sasa hivi ukiwa mtu mzima; jione kama ulivyo sasa hivi ukiwa unamtazama huyo mtoto ambaye umemjengea taswira; mtoto ambaye pia ni wewe. Mtazame na zungumza naye, mwambie ulidanganywa kwamba ni mbaya; huna akili, huna thamani, huwezi, hufai nk; na wewe uliamini kwa sababu ulikuwa mtoto. Lakini sasa umekuwa mkubwa; fahamu ukweli halisi kwamba wewe ni mzuri, una akili unaweza na una thamani sawa na wengine; unaweza na unafaa. Rudia zoezi hili mara kwa mara; kila wakati hakikisha unachagua eneo ambalo uliambiwa huwezi; Futa imani zote mbaya kwenye mawazo yako ya kina.
Tatu
Ni ile ya kufanya zoezi la kurudia rudia maneno pamoja na kujenga taswira mfano: kila wakati jiambie ninaweza; ninafaa; nina thamani, najiamini. Imani ni muhimu sana wakati unajimbia maneno hayo.
Nne
Hapa utaenda kutumia mshumaa, uwashe mshumaa; uweke mbele yako juu ya meza au stuli au sehemu yoyote. Angalia ile sehemu ya mshumaa inayowaka moto (siyo mshumaa wote) kwa muda wa dakika 10, 30 au zaidi. Baada ya hapo fumba macho yako yote ili uuone ule moto wa mshumaa kwa kutumia macho yako ya akili (yaani jicho la tatu). Utaenda kuona moto huo ukiwa wa kijani, bluu, njano au mweupe. Baada ya kuuona, anza kuchoma zile tabia au mambo yanayokukera au kuwakera wengine mfano: Choyo, wivu, uzinzi, dharau, zichome moja baada ya nyingine. Wakati unazichoma utaona moto wa mshumaa ukiongezeka ukubwa au utaona moshi. Fanya zoezi hili mara kwa mara. Baada ya muda utashangaa kuona tabia au mambo hayo yamekwisha na tabia hizo umeziacha kabisa.
Tano
Ni ile hali ya kutumia kioo, simama jitazame kwenye kioo ikiwezekana kila siku asubuhi na jioni. Tafuta zile kasoro ambazo uliambiwa na jiambie kwamba huna. Kama uliambiwa wewe ni mbaya; Basi jiambie wewe ni mzuri, huku ukijiangalia bila kujiogopa kwenye kioo. Lakini kama uliambiwa huwezi, jiambie naweza sana. Pia jikubaai kama ulivyo na jiambie umekamilika, una thamani na unastahili.
Sita
Ni ile hali ya kupata nafasi ya kuyapa mawazo yako ya kawaida baada ya kupewa nafasi ya muda hatimaye yatachukuliwa mawazo yako ya kina, mambo haya mapya yataua au kukausha ile miche/miti iliyoota kwenye mawazo yako ya kina; miti hii ni ile ya mambo ambayo yanakukera au kuwakera wengine. Kwa ile ambayo imeshazaa matunda haiwezi kukauka kwani umeshaanza kuvuna kitu ambacho nidyo maisha unayoishi hivi sasa. Njia hizo zote tano ni za mzunguko. Hii ya sita ni ya njia ya mkato kwani unaenda moja kwa moja kwenye mawazo yako ya kina na kuyaambia yale unayoyahitaji ambayo ni kinyume na yanayokukera.
Nguvu ya uumbaji kitaswira na kujipa nguvu
(i) Kumbuka: Imani – hisia- matokeo
(ii) Ondoa mipango ya zamani kwenye mawazo ya kina ndiyo sababu ya msingi ya kukwama kwani nyuma ni historia na inatia uchungu ukiifikiria.
Kuna aina tatu ya uumbaji kitaswira: sauti, kuona na hisia.
(iv) Kila mmoja ana aina yenye kutawala kwake awe anajua au la. Kuna wengine wanatawaliwa na aina mbili. Katika matumizi ya uumbaji kitaswira, tunaanza na aina yetu, baadaye tunajifunza nyingine.
(v) Ili kujua aina yako, jaribu kufikiria unachohitaji sasa hivi ili uone. Mwanzoni unaweza kusikia sauti inayokuambia hutaweza au ni mzaha ufanyao. Unatakiwa ufanye mazoezi mengi ili uweze kujenga uwezo wako ulionao au uliopotea.
(vi) Mawazo yako ndiyo yenye kukufanya/kukuwezesha ujenge uumbaji kitaswira. Unachokiona kila siku ni matokeo ya kilicho mawazoni kila siku. Hivyo, bila kujua huwa tunaumba yale tusiyoyataka maishani. Uumbaji kitaswira unawakilisha utunzaji wa mbegu (mawazo) kutegemea ni mbegu gani tumepanda.
(vii) Makosa yajitokeza sana; usiweke nguvu kwenye kukosa, kwenye usichotaka na kwenye usichonacho. Mfano: kama umepanga kwenye chumba kimoja na unataka kujenga nyumba yako, usijiambie nimechoka kukaa kwenye haka kakibanda au maisha ya kupanga yamenichosha. Sema lazima niambie nyumbani kwangu yaani nyumba niliyojenga mwenyewe.
(viii) Unapokuwa kwenye uumbaji kitaswira, hisi au ona kama vile jambo limeshakuwa tayari – piga picha ya utayari wa jambo lako.
(ix) Jinsi ya kufanya (hatua);
(i) Tafuta mahali tulivu
(ii) Tuliza mawazo yako
(iii) Weka nguvu zako za mawazo katika jambo unalolitaka
(x) Simamia kufikiria vizuri wakati wote utakaokuwanao na utashangaa kuona matokeo mazuri na kwa muda mfupi sana.
Na: Lusako Mwakiluma
Naamini hiki ni chakula cha siku na mwaka mzima najua utashiba na mwaka 2022 hautakuwa wa hasara kwako. Simamia njia tano ziweze kukubadilisha na kukufanya mpya wakati wote.
Dr Lusako Mwakiluma
Muinuaji na Mhamasishaji
Kwa nini leo nimefikiria haya? Naomba nikwambie pesa ni jawabu la mambo yote namadhambi yote yameanzia kwenye pesa. Unaweza kuwa na rafiki au ndugu mliyeshibana sana lakini pesa ikaja kuwatenganisha kwa urahisi mno na mkachukiana milele. Pesa inatengeza marafiki na pia inaleta uadui ndani yake. Basi ili uishi kwa amani kila kitu unatakiwa ukifanye kwa kiasi.
Kila wakati fanya msaada wa kipesa kama zawadi usifanye kama mkopo. Kama haujampa mtu msaada wa kipesa urafiki wenu unaenda kuisha taratibu. Kama uko kwenye eneo la kuweza kumsaidia mtu basi msaidie usimkopeshe mpe tu. Na kama unajua hauwezi kumpa usimkopeshe itaenda kukuumiza wewe mwenyewe
(Ron Henley).
Sababu ya kutompatia mkopo rafiki au ndugu wa karibu ni kwasababu ya kuondoa usumbufu usio wa lazima wa kudaiana pasipo mashiko. Uhusiano wenu unaenda kuvunjika kama sio kuharibika kabisa. Sababu ya watu inayowapelekea kupata matatizo ya kipesa ni kutojua jinsi ya kufanya kazi na pesa au jinsi ya kutumia fedha. Ukiwakopesha wala hawajui wanaenda kufanyia nini kwani hawajajiandaa cha kwenda kufanyia hizo pesa.
Kabla ya kufahamu hivyo watachukua pesa kwako tena wataanza kutoa udhuru wa kushindwa kukurudishia. Kinachofuata hapo ni kukukimbia kila wanapokuona. Kuacha kupokea simu yako na mwisho kutofungua mlango mara unapopiga hodi majumbani kwao.
Naomba kwa ushauri kama unataka kumsaidia ndugu yako au rafiki mpatie pesa kama msaada na sio mkopo ili uishi kwa amani kwani utakapomkopesha hiyo pesa usiihesabu katika akiba yako kwani imeondoka na hauwezi fahamu itarudi lini.
Hii ni kwa faida yako ya watu wengine.
Karibu tusaidiane pale tuliposhindwa na tunapoweza tuelekezane.
Kwani maarifa ni mali kuliko pesa.
Lusako Mwakiluma
Mhamasishaji na Muinuaji kwa waliokata tamaa na kuugua