JINSI YA KUJITAMBUA MWENYEWE

JINSI YA KUJITAMBUA MWENYEWE

Kama binadamu unatakiwa ujitambue  ili uweze kwenda na wakati au kufanya yale ambayo yanatakiwa  kufanyika  na yale ambayo hayatakiwi kufanyika usiyafanye.

Kuna mambo  ya msingi ya kuyafanya  ili uweze kufikiria  vizuri  wakati wote.  Na kila mtu atakayekuona  atajua huyu mtu amejitambua na amejua  umuhimu wake katika jamii inayomzunguka kwani utajikubali  wakati wote  na kuwaheshimu wengine.

Moja

Fikiri vizuri (jenga mfumo wa kufikiri vizuri); mfumo huu uwe endelevu; siyo usubiri upate tatizo ndiyo uanze kufikiri  vizuri  (usiwe kama zima moto).  Hii itakusaidia  kuanza kupanda mbegu njema kwenye mawazo yako ya kina ili maisha yako ya baadaye  yawe mazuri; yatoe mbegu nzuri/njema.

Mbili

Rudisha mawazo yako nyuma, jenga picha  yako ya utotoni.  Chagua taswira moja wakati ulipokuwa mtoto jione kimwili, kimavazi na mazingira ulipokuwa (nyumbani /shuleni au popote).  Kisha rudi kwako sasa hivi ukiwa mtu mzima; jione kama ulivyo sasa hivi ukiwa unamtazama huyo mtoto ambaye  umemjengea taswira; mtoto ambaye pia ni wewe.  Mtazame  na zungumza  naye, mwambie ulidanganywa kwamba ni mbaya; huna akili, huna thamani, huwezi, hufai nk; na wewe  uliamini kwa sababu ulikuwa mtoto.  Lakini sasa umekuwa mkubwa; fahamu ukweli halisi kwamba wewe ni mzuri, una akili unaweza na una thamani  sawa na wengine; unaweza na unafaa.  Rudia zoezi hili mara kwa mara; kila wakati hakikisha  unachagua  eneo ambalo  uliambiwa  huwezi; Futa  imani zote mbaya kwenye mawazo yako ya kina.

Tatu

Ni ile ya kufanya zoezi la kurudia rudia maneno pamoja na kujenga taswira  mfano: kila wakati  jiambie ninaweza; ninafaa; nina thamani, najiamini.  Imani ni muhimu sana wakati unajimbia maneno hayo.

Nne

Hapa utaenda kutumia mshumaa, uwashe mshumaa; uweke mbele yako juu ya meza au stuli au sehemu yoyote.  Angalia ile sehemu  ya mshumaa inayowaka moto (siyo mshumaa wote) kwa muda wa dakika 10, 30 au zaidi.  Baada ya hapo fumba macho yako yote ili uuone ule moto wa mshumaa  kwa kutumia macho yako ya akili (yaani jicho la tatu).  Utaenda kuona moto huo ukiwa wa kijani, bluu, njano au mweupe.  Baada ya kuuona, anza kuchoma zile tabia  au mambo  yanayokukera au kuwakera  wengine mfano: Choyo, wivu, uzinzi, dharau, zichome  moja baada ya nyingine.  Wakati unazichoma utaona moto wa mshumaa ukiongezeka  ukubwa au utaona moshi.  Fanya zoezi hili mara kwa mara. Baada ya muda utashangaa kuona tabia au mambo hayo yamekwisha na tabia hizo umeziacha kabisa.

Tano

Ni ile hali ya kutumia kioo, simama jitazame kwenye kioo ikiwezekana kila siku asubuhi na jioni.  Tafuta zile kasoro ambazo uliambiwa  na jiambie kwamba huna.  Kama uliambiwa wewe ni mbaya; Basi jiambie wewe ni mzuri, huku ukijiangalia bila kujiogopa kwenye kioo.  Lakini kama uliambiwa huwezi, jiambie naweza sana.  Pia jikubaai kama ulivyo na jiambie umekamilika, una thamani na unastahili.

Sita

Ni ile hali ya kupata nafasi ya kuyapa mawazo yako ya kawaida  baada ya kupewa nafasi ya muda  hatimaye yatachukuliwa mawazo yako ya kina, mambo haya  mapya  yataua au kukausha ile miche/miti iliyoota  kwenye mawazo  yako ya kina; miti hii ni ile ya mambo ambayo yanakukera au kuwakera wengine. Kwa ile ambayo imeshazaa matunda haiwezi kukauka kwani umeshaanza kuvuna kitu ambacho nidyo maisha unayoishi hivi sasa.  Njia hizo zote tano ni za mzunguko.  Hii ya sita  ni ya njia ya mkato kwani unaenda moja kwa moja  kwenye mawazo yako ya kina na kuyaambia yale unayoyahitaji ambayo ni kinyume na yanayokukera.

Nguvu ya uumbaji kitaswira  na kujipa nguvu

(i)                 Kumbuka: Imani – hisia- matokeo

(ii)               Ondoa mipango ya zamani kwenye  mawazo ya kina ndiyo sababu ya msingi ya kukwama kwani nyuma ni historia na inatia uchungu ukiifikiria.

Kuna aina tatu ya uumbaji  kitaswira: sauti, kuona na hisia.

(iv)             Kila mmoja ana aina yenye kutawala kwake awe anajua au la.  Kuna wengine  wanatawaliwa  na aina mbili.  Katika matumizi ya uumbaji kitaswira, tunaanza na aina yetu, baadaye tunajifunza nyingine.

(v)               Ili kujua aina yako, jaribu kufikiria unachohitaji sasa hivi ili uone.  Mwanzoni unaweza kusikia  sauti inayokuambia hutaweza au ni mzaha ufanyao.  Unatakiwa ufanye  mazoezi  mengi ili uweze kujenga uwezo wako ulionao au uliopotea.

(vi)             Mawazo yako ndiyo  yenye  kukufanya/kukuwezesha ujenge uumbaji kitaswira.  Unachokiona kila siku ni matokeo ya kilicho  mawazoni kila siku. Hivyo, bila kujua huwa tunaumba yale tusiyoyataka maishani.  Uumbaji  kitaswira unawakilisha utunzaji wa mbegu (mawazo) kutegemea  ni mbegu gani tumepanda.

(vii)           Makosa  yajitokeza sana; usiweke  nguvu  kwenye kukosa, kwenye usichotaka na kwenye usichonacho.   Mfano: kama umepanga kwenye chumba  kimoja na unataka kujenga nyumba yako, usijiambie nimechoka  kukaa kwenye  haka kakibanda au maisha ya kupanga yamenichosha.  Sema lazima niambie nyumbani kwangu yaani nyumba niliyojenga mwenyewe.

(viii)         Unapokuwa  kwenye uumbaji  kitaswira, hisi au  ona kama vile jambo limeshakuwa  tayari – piga picha ya utayari wa jambo lako.

(ix)                                                                                   Jinsi ya kufanya (hatua);

(i)                 Tafuta mahali tulivu

(ii)               Tuliza mawazo yako

(iii)             Weka nguvu zako  za mawazo  katika jambo  unalolitaka

(x)                Simamia kufikiria vizuri wakati wote utakaokuwanao na utashangaa kuona matokeo mazuri na kwa muda mfupi sana.

Na: Lusako Mwakiluma