Mkurugenzi waWezesha Mabadiliko (WEMA) alikuwa Mgeni Rasmi katika Shule ya Awali Mlali-Morogoro (Bella Day Care).
Mkurugenzi waWezesha Mabadiliko (WEMA) alikuwa Mgeni Rasmi katika Shule ya Awali Mlali-Morogoro (Bella Day Care).
Tambiko la Waluguru lilìfanyika katika Uwanja wa Gofu-Mkoani Morogoro, Mgeni Rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro na aliwakilishwa na Mkuu wa Wilaya Advocate Albert Msando, Mkurugenzi wa Wezesha Dr.Lusako alikuwa mweka hazina wa Tambiko ilo.
Dr. Lusako Mwakiluma aongea kwenye Moro Career Care akizungumzia mahusiano na career
Dr. Lusako Mwakiluma toka Wezesha Mabadiliko Mgeni rasmi Bright Day Care Centre-Morogoro
Na Christina Haule, Morogoro
ZAIDI ya wanafunzi 250 wa shule ya sekondari Uwanja wa Taifa iliyopo Manispaa ya Morogoro wamenufaika na elimu ya utunzaji wa mazingira waliyopewa na Taasisi ya wezesha mabadiliko (WEMA) inayowasaidia kulinda na kutunza mazingira ili kuwaepusha na magojwa ya mlipuko na ya kuambukiza kama vile kipindupindu.
Mkurugenzi wa Taasisi inayojihusisha na kutoa elimu kwa jamii (wezesha mabadiliko, WEMA) Dk.Lusako Mwakiluma alisema kufuatia ongezeko la magonjwa ya mlipuko kwa sasa kama vile U T I na kipindupindu yanayotokana na kuwepo kwa mazingira ya uchafu wameona waitumie nafasi hiyo kutoa elimu kwa wanafunzi hao ili kuifanya shule hiyo kuendeleza usafi na kuwa shule ya mfano kwa shule zingine za Manispaa ya Morogoro
Mkurugenzi huyo alisema pia wamewapatia vifaa mbalimbali vya usafi vyenye thamani ya shilingi milioni moja ambapo alivitaja vifaa hivyo kuwa ni pamoja na mafagio , brashi za kusafishia vyooni, ndoo za kuwekea maji, plastiki za kuwekea takataka na dawa za kusafishia choo.
Alisema kupitia mradi huo waliouita kwa jina la ‘usiupotezee uchafu’ katika shule za sekondari sababu mazingira safi ni maendeleo ambapo mradi huo waliuanzisha baada ya kufanya tafiti na kubaini kuwa katika shule nyingi za sekondari za kata vyoo vyake ni vichafu ambapo kuanzishwa kwa mradi huo kutasaidia wanafunzi kutunza mazingira kwa kusafisha vyoo vyao kila siku ili kuepukana na magonjwa ya UTI na magojwa ya mlipuko kama kipindupindu.
Mwakiluma alisema wataendelea kutoa elimu katika shule zingine nane za Sekondari za kata na baadae kukagua kama wanaendeleza shughuli za utunzaji wa mazingira huku wakiazimia kutoa tuzo kwa shule itakayoendeleza suala zima la utunzaji wa mazingira.
“.Hatuwezi kuweka plasta kidonda bila ya kukiosha ndio mana tumetoa elimu hii ya utunzaji mazingira kwanza kwa kushirikiana nao kwenye usafi na baadae tukatoa vifaa vya kufanyia usafi” alisema Dk. Mwakiluma.
Naye Mwalimu wa nidhamu wa shule hiyo Asifiwe Charles alisema vifaa vilivyotolewa na WEMA vitawasaidia wanafunzi kufanya usafi na kutunza mazingira vyema ili kuepukana na magojwa kwani hapo awali kulikuwa na upungufu wa vifaa kama hivyo shuleni hapo.
Alisema awali shuleni hapo hapakuwa na dastibini za kuwekea taulo za kike mara baada ya kutumika ambapo wasichana walikuwa wakibadilisha pedi zao wanalazimika kutupa katika vyoo na kusababisha kuziba kwa vyoo mara kwa mara na kuingia gharama za kuzibua fedha ambazo zingetumika kwa maendeleo mengine ya shule.
Naye Dada Mkuu wa shule ya sekongari Uwanja wa Taifa Irene Mkondya alisema ataendelea kuwahamasisha wanafunzi wenzie kutunza mazingira kwa maendeleo kwani ameweza kujifunza hasara za kuharibu mazingira kama kutupa taka hovyo kunavyoleta magojwa ya mlipuko kama kuharisha na kipindupindu hivyo aliwasasa wanafunzi wote kutunza mazingira kwani kwa kutunza mazingira watapata maendeleo.
Naye Omari Shabani mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule hiyo alisema elimu waliyopata ya utunzaji wa mazingira itawasaidia katika maisha yao ya kila siku wawapo mashuleni na hata majumbani kwa sababu wanaweza kutunza mazingira kwa maendeleo.
Hivyo aliwasihi wanafunzi kuendelea kutunza mazingira ili kuepukana na magojwa ambayo yanaweza kuwakalisha chini na kuwafanya kushindwa kuendelea na masomo lakini pia kushindwa kuendelea na shughuli zao za maendeleo hapo baadae wakiwa wameshaanza kazi.
Taasisi ya wezesha mabadiliko hutoa elimu ya kujitambua kwa vijana na wanafunzi, elimu ya afya ya uzazi, jinsi ya kuepuka mimba na ndoa za utotoni na jinsi ya kuepuka TB, Ugonjwa wa upungufu wa kinga mwilini(UKIMWI) na kwamba kwa sasa inatekeleza mradi wa miezi nane katika shule 8 za sekondari za kata zilizopo manispaa ya Morogoro.
HAFLA YA UGAWAJI WA TAULO ZA MTOTO WA KIKE KATIKA SHULE ZA SEKONDARI MANISPAA YA MOROGORO KWA WANAFUNZI WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU
a
AFISA MAENDELEO YA JAMII NA MRATIBU WA DAWATI LA MAENDELEO YA MTOTO MANISPAA YA MOROGORO , JOYCE MUGAMBI, AKIZUNGUMZA KWA NIABA YA MKURUGENZI WA MANISPAA YA MOROGORO KATIKA HAFLA YA UGAWAJI WA TAULO ZA MTOTO WA KIKE KATIKA SHULE ZA SEKONDARI MANISPAA YA MOROGORO KWA WANAFUNZI WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU.
HAFLA HIYO IMEFANYIKA MEI 21 /2022 KATIKA UKUMBI WA MIKUTANO WA KILAKALA SOKO KUU LA CHIFU KINGALU MOROGORO.
TAULO HIZO ZIMETOLEWA NA TAASISI YA WEZESHA MABADILIKO CHINI YA MKURUGENZI WAKE DR. LUSAKO MWAKILUMA.🙏🏻🙏🏻🙏🏻🔥🔥🔥
Kama binadamu unatakiwa ujitambue ili uweze kwenda na wakati au kufanya yale ambayo yanatakiwa kufanyika na yale ambayo hayatakiwi kufanyika usiyafanye.
Kuna mambo ya msingi ya kuyafanya ili uweze kufikiria vizuri wakati wote. Na kila mtu atakayekuona atajua huyu mtu amejitambua na amejua umuhimu wake katika jamii inayomzunguka kwani utajikubali wakati wote na kuwaheshimu wengine.
Moja
Fikiri vizuri (jenga mfumo wa kufikiri vizuri); mfumo huu uwe endelevu; siyo usubiri upate tatizo ndiyo uanze kufikiri vizuri (usiwe kama zima moto). Hii itakusaidia kuanza kupanda mbegu njema kwenye mawazo yako ya kina ili maisha yako ya baadaye yawe mazuri; yatoe mbegu nzuri/njema.
Mbili
Rudisha mawazo yako nyuma, jenga picha yako ya utotoni. Chagua taswira moja wakati ulipokuwa mtoto jione kimwili, kimavazi na mazingira ulipokuwa (nyumbani /shuleni au popote). Kisha rudi kwako sasa hivi ukiwa mtu mzima; jione kama ulivyo sasa hivi ukiwa unamtazama huyo mtoto ambaye umemjengea taswira; mtoto ambaye pia ni wewe. Mtazame na zungumza naye, mwambie ulidanganywa kwamba ni mbaya; huna akili, huna thamani, huwezi, hufai nk; na wewe uliamini kwa sababu ulikuwa mtoto. Lakini sasa umekuwa mkubwa; fahamu ukweli halisi kwamba wewe ni mzuri, una akili unaweza na una thamani sawa na wengine; unaweza na unafaa. Rudia zoezi hili mara kwa mara; kila wakati hakikisha unachagua eneo ambalo uliambiwa huwezi; Futa imani zote mbaya kwenye mawazo yako ya kina.
Tatu
Ni ile ya kufanya zoezi la kurudia rudia maneno pamoja na kujenga taswira mfano: kila wakati jiambie ninaweza; ninafaa; nina thamani, najiamini. Imani ni muhimu sana wakati unajimbia maneno hayo.
Nne
Hapa utaenda kutumia mshumaa, uwashe mshumaa; uweke mbele yako juu ya meza au stuli au sehemu yoyote. Angalia ile sehemu ya mshumaa inayowaka moto (siyo mshumaa wote) kwa muda wa dakika 10, 30 au zaidi. Baada ya hapo fumba macho yako yote ili uuone ule moto wa mshumaa kwa kutumia macho yako ya akili (yaani jicho la tatu). Utaenda kuona moto huo ukiwa wa kijani, bluu, njano au mweupe. Baada ya kuuona, anza kuchoma zile tabia au mambo yanayokukera au kuwakera wengine mfano: Choyo, wivu, uzinzi, dharau, zichome moja baada ya nyingine. Wakati unazichoma utaona moto wa mshumaa ukiongezeka ukubwa au utaona moshi. Fanya zoezi hili mara kwa mara. Baada ya muda utashangaa kuona tabia au mambo hayo yamekwisha na tabia hizo umeziacha kabisa.
Tano
Ni ile hali ya kutumia kioo, simama jitazame kwenye kioo ikiwezekana kila siku asubuhi na jioni. Tafuta zile kasoro ambazo uliambiwa na jiambie kwamba huna. Kama uliambiwa wewe ni mbaya; Basi jiambie wewe ni mzuri, huku ukijiangalia bila kujiogopa kwenye kioo. Lakini kama uliambiwa huwezi, jiambie naweza sana. Pia jikubaai kama ulivyo na jiambie umekamilika, una thamani na unastahili.
Sita
Ni ile hali ya kupata nafasi ya kuyapa mawazo yako ya kawaida baada ya kupewa nafasi ya muda hatimaye yatachukuliwa mawazo yako ya kina, mambo haya mapya yataua au kukausha ile miche/miti iliyoota kwenye mawazo yako ya kina; miti hii ni ile ya mambo ambayo yanakukera au kuwakera wengine. Kwa ile ambayo imeshazaa matunda haiwezi kukauka kwani umeshaanza kuvuna kitu ambacho nidyo maisha unayoishi hivi sasa. Njia hizo zote tano ni za mzunguko. Hii ya sita ni ya njia ya mkato kwani unaenda moja kwa moja kwenye mawazo yako ya kina na kuyaambia yale unayoyahitaji ambayo ni kinyume na yanayokukera.
Nguvu ya uumbaji kitaswira na kujipa nguvu
(i) Kumbuka: Imani – hisia- matokeo
(ii) Ondoa mipango ya zamani kwenye mawazo ya kina ndiyo sababu ya msingi ya kukwama kwani nyuma ni historia na inatia uchungu ukiifikiria.
Kuna aina tatu ya uumbaji kitaswira: sauti, kuona na hisia.
(iv) Kila mmoja ana aina yenye kutawala kwake awe anajua au la. Kuna wengine wanatawaliwa na aina mbili. Katika matumizi ya uumbaji kitaswira, tunaanza na aina yetu, baadaye tunajifunza nyingine.
(v) Ili kujua aina yako, jaribu kufikiria unachohitaji sasa hivi ili uone. Mwanzoni unaweza kusikia sauti inayokuambia hutaweza au ni mzaha ufanyao. Unatakiwa ufanye mazoezi mengi ili uweze kujenga uwezo wako ulionao au uliopotea.
(vi) Mawazo yako ndiyo yenye kukufanya/kukuwezesha ujenge uumbaji kitaswira. Unachokiona kila siku ni matokeo ya kilicho mawazoni kila siku. Hivyo, bila kujua huwa tunaumba yale tusiyoyataka maishani. Uumbaji kitaswira unawakilisha utunzaji wa mbegu (mawazo) kutegemea ni mbegu gani tumepanda.
(vii) Makosa yajitokeza sana; usiweke nguvu kwenye kukosa, kwenye usichotaka na kwenye usichonacho. Mfano: kama umepanga kwenye chumba kimoja na unataka kujenga nyumba yako, usijiambie nimechoka kukaa kwenye haka kakibanda au maisha ya kupanga yamenichosha. Sema lazima niambie nyumbani kwangu yaani nyumba niliyojenga mwenyewe.
(viii) Unapokuwa kwenye uumbaji kitaswira, hisi au ona kama vile jambo limeshakuwa tayari – piga picha ya utayari wa jambo lako.
(ix) Jinsi ya kufanya (hatua);
(i) Tafuta mahali tulivu
(ii) Tuliza mawazo yako
(iii) Weka nguvu zako za mawazo katika jambo unalolitaka
(x) Simamia kufikiria vizuri wakati wote utakaokuwanao na utashangaa kuona matokeo mazuri na kwa muda mfupi sana.
Na: Lusako Mwakiluma
Naamini hiki ni chakula cha siku na mwaka mzima najua utashiba na mwaka 2022 hautakuwa wa hasara kwako. Simamia njia tano ziweze kukubadilisha na kukufanya mpya wakati wote.
Dr Lusako Mwakiluma
Muinuaji na Mhamasishaji
Choo cha Mtoto wa Kike Shule ya Sekondari Uluguru ,kilichofadhiliwa na Taasisi ya WEZESHA MABADILIKO.
Mkurugenzi wa WEZESHA MABADILIKO, Dr. Lusako Mwakiluma (kushoto), akisalimia na Afisa Elimu Taaluma Msingi Manispaa ya Morogoro, Leah Selemani (kulia) mara baada ya uzinduiz wa Choo cha Mtoto wa Kike.
Mkurugenzi wa WEZESHA MABADILIKO, Dr. Lusako Mwakiluma (watatu kutoka kushoto) , Mtendaji wa Kata ya Kihonda Tatu Ally (kushoto) wakiwa na Wanafunzi mara baada ya uzinduzi wa Choo cha Mtoto wa Kike.
Mkurugenzi wa WEZESHA MABADILIKO, Dr. Lusako Mwakiluma (watatu kutoka kushoto),akimkabidhi ndoo ya kunawia maji Afisa Elimu Taaluma Msingi Manispaa ya Morogoro, Leah Selemani (kulia).
TAASISI isiyo ya Kiserikali ya WEZEESHA MABADILIKO chini ya Mkurugenzi wake. Dr. Lusako Mwakiluma,imeikabidhi Manispaa ya Morogoro Choo cha Mtoto wa Kike katika Shule ya Sekondari Uluguru.
Tukio hilo la makabidhiano ya Choo limefanyika hivi karibuni ambapo Choo hicho katika makabidhiano kilipokelewa na Mwakailishi wa Mkurugenzi kutoka idara ya elimu Msingi, Leah Selemani.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi choo hicho, Mkurugenzi wa WEZESHA MABADILIKO, Dr. Lusako, amesema kwa kuwa wanawake wengi wamekuwa na changamoto nyingi katika mabadiliko ya kimwili hivyo wameona kujenga Choo cha Mtoto itakuwa ni suluhisho la kuwaondolea adha wanafunzi wakike wanapoingia katika hedhi.
Dr. Lusako,amesema kuwa tafiti zinaonesha kuwa mtoto wa kike anakosa masomo siku 4 hadi 5 kila mwezi kutokana na ukosefu wa huduma ya vyoo bora na maji salama na safi shuleni ambapo Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizosaini mkataba wa Malengo ya Maendeleo Endelevu ifikapo mwaka 2030. Miongoni mwa malengo hayo ni lile lengo namba 4: linalohamasisha kuhusu Elimu Bora, Lengo la 5: linalo hamasisha juu ya Usawa wa Kijinsi na lengo namba 6: kuhusu Maji Safi na Salama.
“Huu ni mwanzo tu bado tuna malengo ya kusaidia na shule nyengine , tunataka choo hiki kiwe cha mfano katika Manispaa yetu ya Morogoro , tuliona kuna Choo Tubuyu Sekondari lakini kuna chengine hakijaisha pale Kihonda Sekondari, sisi baada ya kuguswa na jitihada hizi, tumeona nasisi tuunge mkono jitihada za Manispaa yetu kwa kuwajengea Choo hiki cha Kisasa ili kuhakikisha mtoto wa kike anawekewa mazingira rafiki anapokuwa shuleni ili aweze kuhudhuria siku za masomo kwa ukamilifu kama ilivyokuwa kwa mtoto wa kiume kwani “Ukimkomboa mtoto wa kike umekomboa Taifa zima” Ameongeza Dr. Lusako.
Aidha, amesema kuguswa kwao katika ujenzi wa Vyoo vya Mtoto wa kike imetokana na changamoto zinazoendelea kuwakabili wanafunzi kukosa vyoo bora na maji salama na safi shuleni. Tatizo hili linawaathiri watoto wa kike zaidi kwani wanashindwa kujistiri hasa wanapokuwa katika siku zao za hedhi katika mazingira ya shuleni.
Naye Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro,ambaye pia ni afisa Taaluma Msingi, Leah Selemani, amempongeza Mkurugenzi wa WEZESHA MABADILIKO kwa kuwasaidia wanafunzi wa kike shuleni.
Amesema Vyoo hivyo vitapunguza utoro kwa watoto wa kike kwani wengi wamekuwa wakishindwa kufika shule wakati wa hedhi lakini baada ya ujenzi huo utasaidia sana na wanafunzi watahuduhuria shule wakiwa katika hali hiyo maana ipo sehemu salama kwao katika kujisafisha na kujilinda.
Mama Selemani , ameowaomba Wazazi kuwahimiza watoto kwenda shule mara baada ya kupata hedhi kwani mabadiliko hayo yanazuilika wakiwa shuleni.
“Dada yetu Dr. Lusako, amefanya jambo zuri sana, sisi kama Manispaa tunampongeza sana kwa jitihada zake, hii ni mbinu nzuri sana , hiki ni choo cha 3 kwa Manispaa yetu, kimoja kipo Tubuyu Sekondari, kingine kipo Kihonda Sekondari hakijaisha na mategemeo yetu kiishe mwaka huu unaokuja wa 2022, choo hiki kitasaidia kupunguza utoro kwa watoto wa kike wanaoingia katika siku zao (hedhi), kumekuwa na changamoto wanafunzi kubeba pedi kwenye begi na kwenda nazo shule wengine wanaenda kuomba ofisini , lakini kwa hali hii ni vigumu hata kutambua mtu yupo katika hali gani maana vifaa vyote vitakuwa chooni ni yeye kwenda na kujihudumia”Amesema Mama Selemani.
Kwa nini leo nimefikiria haya? Naomba nikwambie pesa ni jawabu la mambo yote namadhambi yote yameanzia kwenye pesa. Unaweza kuwa na rafiki au ndugu mliyeshibana sana lakini pesa ikaja kuwatenganisha kwa urahisi mno na mkachukiana milele. Pesa inatengeza marafiki na pia inaleta uadui ndani yake. Basi ili uishi kwa amani kila kitu unatakiwa ukifanye kwa kiasi.
Kila wakati fanya msaada wa kipesa kama zawadi usifanye kama mkopo. Kama haujampa mtu msaada wa kipesa urafiki wenu unaenda kuisha taratibu. Kama uko kwenye eneo la kuweza kumsaidia mtu basi msaidie usimkopeshe mpe tu. Na kama unajua hauwezi kumpa usimkopeshe itaenda kukuumiza wewe mwenyewe
(Ron Henley).
Sababu ya kutompatia mkopo rafiki au ndugu wa karibu ni kwasababu ya kuondoa usumbufu usio wa lazima wa kudaiana pasipo mashiko. Uhusiano wenu unaenda kuvunjika kama sio kuharibika kabisa. Sababu ya watu inayowapelekea kupata matatizo ya kipesa ni kutojua jinsi ya kufanya kazi na pesa au jinsi ya kutumia fedha. Ukiwakopesha wala hawajui wanaenda kufanyia nini kwani hawajajiandaa cha kwenda kufanyia hizo pesa.
Kabla ya kufahamu hivyo watachukua pesa kwako tena wataanza kutoa udhuru wa kushindwa kukurudishia. Kinachofuata hapo ni kukukimbia kila wanapokuona. Kuacha kupokea simu yako na mwisho kutofungua mlango mara unapopiga hodi majumbani kwao.
Naomba kwa ushauri kama unataka kumsaidia ndugu yako au rafiki mpatie pesa kama msaada na sio mkopo ili uishi kwa amani kwani utakapomkopesha hiyo pesa usiihesabu katika akiba yako kwani imeondoka na hauwezi fahamu itarudi lini.
Hii ni kwa faida yako ya watu wengine.
Karibu tusaidiane pale tuliposhindwa na tunapoweza tuelekezane.
Kwani maarifa ni mali kuliko pesa.
Lusako Mwakiluma
Mhamasishaji na Muinuaji kwa waliokata tamaa na kuugua